Ulimwengu

Qatar yasisitiza utekelezwaji kamili wa kusitishwa mapigano Gaza
Qatar inaendelea kusisitiza mpango wa utekelezwaji kamili wa usitishwaji mapigano Gaza licha ya upinzani wa Israel, huku ikitoa wito wa kumaliza hali ya taharuki kote katika kanda na kuanzishwa tena kwa mazungumzo kati ya Marekani na Iran.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, anasema Tehran ilipambana kwa masharti yake yenyewe na kuwalazimu wale waliotaka “isalimu amri bila masharti” kufanya mazungumzo, baada ya Donald Trump kuitaka Iran “kuinua bendera nyeupe.”
Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amewaomba viongozi wa nchi za ukanda huo siku ya Jumatatu kushirikiana katika kukabiliana na suala la wahamiaji wanaokwenda Afrika Kusini.
Rais wa Marekani anasema wanafanya mawasiliano ya moja kwa moja na kikosi cha IRGC cha Iran na kutishia Oman kuhusu hatua yake katika majadiliano, huku akitoa wito kwa Israel kusitishga mashambulizi Gaza.
Afrika

Jaji wa Marekani aruhusu serikali kufuta hadhi ya kinga kwa raia wa Ethiopia
Jaji wa mahakama ya Boston nchini Marekani siku ya Jumanne aliruhusu serikali ya Trump kuwaondolea kinga ya kupinga kurudishwa kwao raia karibu 5,000 wa Ethiopia.
Watu zaidi ya 5,000 walioondolewa katika makazi yao kutokana na mashambulizi ya wapiganaji wa RSF nchini Sudan wamewasili Damazin, mji mkuu wa jimbo la kusini mashariki la Blue Nile.
Plateau, lililoko katikati mwa Nigeria, limekumbwa na vurugu zinazohusishwa na migogoro ya ardhi, maeneo ya malisho na raslimali zingine.
Kamati ya Dharura ya WHO inakutana siku ya Jumanne kujadili mlipuko huo, ambao ulitangazwa kuwa dharura ya kimataifa.
Michezo

















