DRC yaaga Kombe la Dunia baada ya kufungwa na England

Mwisho wa safari! Timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imeaga Kombe la Dunia baada ya kupoteza 2-1 dhidi ya England.

Newstimehub

Newstimehub

2 Julai, 2026

e6c2f55f39c4f428d0933b39b93362ae3eeeea6ac6686e6e6036996873c4940e main

Mshambuliaji wa England, Harry Kane, alifunga mabao mawili katika dakika za mwisho na kuiongoza timu yake kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), na hivyo kuitoa kwenye Kombe la Dunia 2026 katika hatua ya mtoano ya timu 32 bora.

Mechi hio iliochezwa Jumatano jijini Atlanta, Marekani, ilianza kwa kasi huku DRC ikitangulia kufunga kupitia bao la Brian Cipenga aliyetikisa nyavu katika dakika ya saba.

Kwa ushindi huo, England imefuzu hatua ya 16 bora, ambapo itakutana na Mexico katika mechi itakayochezwa Jumapili jijini Mexico City.