Kenya, Uturuki kushirikiana zaidi katika biashara, uwekezaji na ulinzi

Kenya inataka uwekezaji zaidi kutoka Uturuki, ikiwemo ushirikiano katika sekta ya anga huku Uturuki ikijitolea ushirikiano katika masuala ya kupambana na ugaidi, ulinzi na utulivu wa kanda

Newstimehub

Newstimehub

19 Agosti, 2026

07a48b01 8b2b 4e05 9d46 825b83e64c4f 1787133969632

Kenya na Uturuki zimedhamiria kuboresha uhusiano wao zaidi ya ushirikiano wa kidiplomasia wa muda mrefu, huku zikilenga ushirikiano katika biashara, uwekezaji, anga, ulinzi na utulivu wa kanda, amesema Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Jumatano.

Majadiliano yamefanyika jijini Nairobi kati ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Musalia Mudavadi na Wabunge Marafiki kati ya Uturuki na Kenya.

“Ushirika wenye nguvu wa kimataifa unatakiwa kufungua milango ya biashara za Kenya, kutengeza ajira na kuunganisha watu katika masoko makubwa,” amesema Mudavadi baada ya mkutano huo.

Kwa mujibu wa Wizara, Kenya inataka kuongezeka kwa uwekezaji wa Uturuki na ushirikiano mkubwa wa biashara, hasa katika viwanda, utalii na masuala ya anga, wakati ambapo Kenya inatizamia kuboresha nafasi yake kama mlango mkuu wa biashara katika eneo la Afrika Mashariki.

Pande hizo mbili pia zilijadili ushirikiano kati ya Shirika la Ndege la Kenya na Shirika la Ndege la Uturuki, kwa kuongeza safari ambazo zinarahisisha utalii, uwekezaji na safari za kibiashara kati ya nchi hizo mbili.

Ujumbe wa Uturuki uliongozwa na Ismail Gunes, mbunge wa Bunge la Uturuki kutoka mkoa wa Usak na mwenyekiti mwenza wa Wabunge Marafiki kati ya Uturuki na Kenya.

Kwa upande wake, ujumbe wa Kenya uliongozwa na mbunge Adan Keynan Wehliye, ambae ni mwenyekiti wa umoja huo wa wabunge.