Tanzania yatoa tahadhari ya mvua za El Nino

Kulingana na Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Ladislaus Chang’a, mvua hizo zinatarajiwa kuanza katika wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Oktoba katika baadhi ya mikoa nchini humo.

Newstimehub

Newstimehub

19 Agosti, 2026

2471d24f 3066 47e7 81a3 9fd8271a6115 1787129506274

 Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania (TMA), imesema mvua za msimu wa vuli za Oktoba hadi Desemba 2026, zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mbalimbali nchini, huku uwepo wa mvua kubwa  ( El Nino), ukitajwa kuwa miongoni mwa sababu zinazoweza kuchangia vipindi vya mvua kubwa katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo.

Kulingana na Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Ladislaus Chang’a, mvua hizo zinatarajiwa kuanza katika wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Oktoba katika baadhi ya mikoa nchini humo.

Chang’a alisema kuwa, katika mikoa ya Arusha na Manyara, mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani, huku hali kama hiyo ikitarajiwa pia katika ukanda wa Kaskazini unaojumuisha Tanga, Dar es Salaam, kaskazini mwa Morogoro pamoja na visiwa vya Mafia na Pemba.

Kwa mujibu wa TMA, uwepo wa mvua za El Nino unaweza kuchangia kuongezeka kwa vipindi vya mvua kubwa, hali ambayo inaweza kusababisha mafuriko na athari katika miundombinu, kilimo, usafiri na shughuli nyingine za kijamii na kiuchumi.