Serikali ya Rwanda kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), limepokea wakimbizi wa kisiasa 177, waliokuwa wametafuta hifadhi nchini Libya.
Watu hao, wanahusisha raia wa mataifa mbalimbali, yakiwemo Sudan, Eritrea, Somalia, Ethiopia na Sudan Kusini.
Kulingana na serikali ya nchi hiyo, watu hao watahifadhiwa katika kituo cha Gashora kilichopo katika wilaya ya Gashora, wakisubiria kupelekwa mataifa mengine.
Kufikia sasa, idadi ya wakimbizi wa kisiasa waliopokelewa Rwanda, imefikia zaidi ya 3,000.
Uhamisho wa wakimbizi hao wa kisiasa ni sehemu ya makubaliano kati ya UNHCR na Umoja wa Afrika, kwa lengo la kuwaisaidia wakimbizi waliokwama Libya.















