Bunge la Senegal lapitisha sheria inayomtaka rais kutangaza mali zake anapochaguliwa na anapoondoka

Bunge la Senegal limepitisha sheria inayomtaka rais, spika, na waziri mkuu kutangaza mali zao wanapoingia kwenye uongozi na wakati wanapoondoka madarakani.

Newstimehub

Newstimehub

17 Agosti, 2026

cfa00af3 5afa 4c65 a60a 66319273e32d 1786990999540

Bunge la Senegal siku ya Jumatatu limepitisha sheria inayomtaka rais, spika, na waziri mkuu kutangaza mali zao wanapoingia kwenye uongozi na wakati wanapoondoka madarakani.

Sheria hiyo mpya ina lengo la kuimarisha uwazi, ahadi iliyotolewa na serikali ilioko uongozini ambayo iliingia madarakani Aprili 2024 baada ya miaka 12 chini ya uongozi wa Rais Macky Sall.

Lakini inakuja baada ya Rais Bassirou Diomaye Faye kumtimua aliyekuwa waziri mkuu wake Ousmane Sonko Mei 2026.

Kutangaza mali ilikuwa ni kwa mujibu wa katiba tangu 2001 lakini inatakelezwa tu wakati mtu anapoingia madarakani.

Wabunge 133 kati ya 165 waidhinisha

Kwa mujibu wa sheria hii mpya, viongozi hao inabidi watangaze mali zao miezi mitatu baada ya kuingia uongozini na ndani ya miezi mitatu ya kuondoka madarakani.

Sheria hiyo, iliyowasilishwa na wengi wa wabunge wanaoongozwa na Sonko, kwanza ilimlenga rais pekee lakini ikaimarishwa kujumuisha spika wa bunge na waziri mkuu.

Ilipitishwa siku ya Jumatatu na wabunge 133 kati ya 165.

‘Mtazamo kamili’

Waziri wa Sheria Moussa Sarr alisema siku ya Jumatatu kuwa mabadiliko yanatakiwa kuwa “sehemu ya mtazamo kamili” ambayo “yatatekelezwa” iwapo yatajumuishwa katika kura ya maoni kuhusu katiba.

Faye, ambaye alikuwa kiongozi mwandamizi wa zamani wa chama cha Pastef, alitangaza mwezi Juni mpango wa kufanyika kwa kura ya maoni kuhusu katiba, ingawa bado tarehe haijatangazwa.

Wakati huohuo, Sonko alitangazwa spika wa bunge linaloongozwa na chama cha Pastef baada ya kufutwa uwaziri mkuu.

Rais Faye naye akaunda chama chake cha kisiasa mwishoni mwa mwezi Julai 2026.