Ulimwengu

243a112c 169a 4b7b 9e4b 9cd2ac76a6ae 1787072973188

Qatar yasisitiza utekelezwaji kamili wa kusitishwa mapigano Gaza

Qatar inaendelea kusisitiza mpango wa utekelezwaji kamili wa usitishwaji mapigano Gaza licha ya upinzani wa Israel, huku ikitoa wito wa kumaliza hali ya taharuki kote katika kanda na kuanzishwa tena kwa mazungumzo kati ya Marekani na Iran.

Iran yasema imeshinda katika vita na diplomasia baada ya Trump kuitaka ijisalimishe

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, anasema Tehran ilipambana kwa masharti yake yenyewe na kuwalazimu wale waliotaka “isalimu amri bila masharti” kufanya mazungumzo, baada ya Donald Trump kuitaka Iran “kuinua bendera nyeupe.”

Afrika Kusini yataka viongozi kuungana kushughulikia changamoto ya uhamiaji

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amewaomba viongozi wa nchi za ukanda huo siku ya Jumatatu kushirikiana katika kukabiliana na suala la wahamiaji wanaokwenda Afrika Kusini.

Trump atishia kuishambulia Oman iwapo ‘itakwamisha’ mazungumzo ya Marekani na Iran

Rais wa Marekani anasema wanafanya mawasiliano ya moja kwa moja na kikosi cha IRGC cha Iran na kutishia Oman kuhusu hatua yake katika majadiliano, huku akitoa wito kwa Israel kusitishga mashambulizi Gaza.

Afrika

20e403e5 7744 4204 9faf 2cf7686ab89d 1787079981559

Jaji wa Marekani aruhusu serikali kufuta hadhi ya kinga kwa raia wa Ethiopia

Jaji wa mahakama ya Boston nchini Marekani siku ya Jumanne aliruhusu serikali ya Trump kuwaondolea kinga ya kupinga kurudishwa kwao raia karibu 5,000 wa Ethiopia.

Zaidi ya watu 5,000 walioondolewa katika makazi yao wawasili mji mkuu wa jimbo la Blue Nile

Watu zaidi ya 5,000 walioondolewa katika makazi yao kutokana na mashambulizi ya wapiganaji wa RSF nchini Sudan wamewasili Damazin, mji mkuu wa jimbo la kusini mashariki la Blue Nile.

Nigeria yachunguza mauaji yaliyosababisha vifo vya watu wasiopungua 25 katika jimbo la Plateau

Plateau, lililoko katikati mwa Nigeria, limekumbwa na vurugu zinazohusishwa na migogoro ya ardhi, maeneo ya malisho na raslimali zingine.

Mlipuko wa Ebola nchini Congo unaweza kudhibitiwa ndani ya miezi mitatu: WHO

Kamati ya Dharura ya WHO inakutana siku ya Jumanne kujadili mlipuko huo, ambao ulitangazwa kuwa dharura ya kimataifa.