Ulimwengu

570af43d 439f 47f6 8807 93d4577960bb 1787048078684

Iran yasema imeshinda katika vita na diplomasia baada ya Trump kuitaka ijisalimishe

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, anasema Tehran ilipambana kwa masharti yake yenyewe na kuwalazimu wale waliotaka “isalimu amri bila masharti” kufanya mazungumzo, baada ya Donald Trump kuitaka Iran “kuinua bendera nyeupe.”

Afrika Kusini yataka viongozi kuungana kushughulikia changamoto ya uhamiaji

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amewaomba viongozi wa nchi za ukanda huo siku ya Jumatatu kushirikiana katika kukabiliana na suala la wahamiaji wanaokwenda Afrika Kusini.

Trump atishia kuishambulia Oman iwapo ‘itakwamisha’ mazungumzo ya Marekani na Iran

Rais wa Marekani anasema wanafanya mawasiliano ya moja kwa moja na kikosi cha IRGC cha Iran na kutishia Oman kuhusu hatua yake katika majadiliano, huku akitoa wito kwa Israel kusitishga mashambulizi Gaza.

Trump afurahishwa na mkataba wa ulinzi wa Makkah uliosainiwa na Uturuki, Pakistan na Saudi Arabia

Rais wa Marekani amepongeza makubaliano hayo muhimu kama hatua kubwa ya kwanza kuelekea ushirikiano mkubwa zaidi wa kikanda na ulinzi imara wa pamoja katika Mashariki ya Kati, huku akiwapongeza viongozi wa nchi hizo tatu.

Afrika

75d3cf87 336d 4241 a4db 6c5229eb4cd5 1787036433868

Hichilema ashinda Uchaguzi wa Zambia

Ushindi huo umemuwezesha Hichilema kuvuka kizingiti cha kikatiba cha kupata zaidi ya asilimia 50.

Bunge la Senegal lapitisha sheria inayomtaka rais kutangaza mali zake anapochaguliwa na anapoondoka

Bunge la Senegal limepitisha sheria inayomtaka rais, spika, na waziri mkuu kutangaza mali zao wanapoingia kwenye uongozi na wakati wanapoondoka madarakani.

Hatma ya Tundu Lissu kujulikana Agosti 21

Lissu anakabiliwa na shtaka moja la uhaini kinyume na kifungu cha 39(2)(d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, linalohusishwa na maneno aliyodaiwa kuyatamka kuhusu kusudio la kuzuia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Mkosoaji wa serikali ya kijeshi ya Mali atupwa jela miaka 7

Toka iingie madarakani, serikali ya kijeshi ya nchi hiyo, imethibiti kwa kiasi kikubwa, uhuru wa kutoa maoni, ikiwemo na kufuta utaratibu wa vyama vya kisiasa.