Mkosoaji wa serikali ya kijeshi ya Mali atupwa jela miaka 7

Toka iingie madarakani, serikali ya kijeshi ya nchi hiyo, imethibiti kwa kiasi kikubwa, uhuru wa kutoa maoni, ikiwemo na kufuta utaratibu wa vyama vya kisiasa.

Newstimehub

Newstimehub

17 Agosti, 2026

f2ce4ee7 c5c1 4a06 9a91 58a270725462 1786968210901

Mahakama ya Mali imemhukumu kifungo cha miaka saba jela, mtangazaji na mtengeneza maudhui maarufu nchini humo, Mohamed Youssouf Bathily kwa kukosoa serikali ya kijeshi iliyopo madarakani.

Bathily, maarufu kama Ras Bath, amehukumiwa kwa kupanga njama za kuikosoa serikali ya Mali, akishirikiana na Rokia Doumbia.

Wawili hao, walikuwa kizuizini kwa kipindi kirefu, baada ya kurusha kipindi cha mwaka 2023, kinachoangazia hali ya uchumi wa Mali.

Waendesha mashitaka wa nchi hiyo, waliiambia mahakama ya jijini Bamako kuwa, “Ras Bath” ni tishio kwa serikali ya Mali, na ni vyema awekwe mbali na matumizi ya mitandao ya kijamii na redio.

Hata hivyo, wanasheria wake wamekana madai hayo.

Toka iingie madarakani, serikali ya kijeshi ya nchi hiyo, imethibiti kwa kiasi kikubwa, uhuru wa kutoa maoni, ikiwemo na kufuta utaratibu wa vyama vya kisiasa.