Netanyahu: Vita vya Iran bado havijaisha

Kauli yake, aliyoitoa siku ya Alhamisi, inafuatia mfululilizo wa mashambulizi yaliyofanywa na Marekani dhidi ya Iran, katika kipindi cha siku mbili.

Newstimehub

Newstimehub

9 Julai, 2026

66711678 5e68 4700 95a8 d877d2a58598 1776171031337

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ameweka wazi kuwa, vita dhidi ya taifa la Iran bado havijaisha.

Kauli yake, aliyoitoa siku ya Alhamisi, inafuatia mfululilizo wa mashambulizi yaliyofanywa na Marekani dhidi ya Iran, katika kipindi cha siku mbili.

“Vita bado havijaisha, bado kuna changamoto mpya ambazo tunakabaliana nazo,” alisema Netanyahu wakati wa mahafali ya chuo cha anga cha Hatzerim cha nchini Israel.

Iran na Marekani ziliishambuliana siku mbili zilizopita, baada ya Iran kudaiwa kushambulia meli tatu katika Mlango Bahari wa Hormuz.

Kwa upande wake, Mnadhimu Mkuu wa Majeshi wa Israel, Eyal Zamir amesema kuwa kampeni ya kijeshi dhidi ya Iran bado haijamalizika.

 “Bado tuna mipango mipya ambayo tumeiandaa, katika siku zijazo,” alisema.