Korea Kusini imedai kuwa, ndege za kivita za Urusi zimeingilia anga yake, ikitengua kauli yake ya awali kuwa zilikuwa ni ndege za Korea Kaskazini.
“Ilikuwa ni ndege ya Kirusi iliyovunja sheria na kukiuka taratibu za anga,” ilisema serikali ya nchi hiyo.
Hapo awali, vyombo vya habari mbalimbali vya Korea Kusini, viliituhumu Korea Kaskazini, kabla ya kubadilisha taarifa yao.
“Taarifa zinazodai kuwa ni ndege kutoka Korea Kaskazini hazina ukweli wowote,” ilisema taarifa hiyo.
Muda mfupi baadaye, Korea Kusini ilidai kuwa ilikuwa ni ndege ya kijeshi ya Urusi iliyoingia kwenye anga yake.
Serikali ya nchi hiyo, imesisitiza haja ya kumuita mwambata wa kijeshi wa Urusi nchini humo, kuzungumzia suala hilo.















