Mkuu wa ujasusi wa wapiganaji wa RSF ajiunga na upande wa jeshi la Sudan

Al-Tayeb Jabara ameomba radhi kwa kujiunga na RSF, akisema kuwa yuko tayari kusaidia jeshi katika mapambano dhidi ya wapiganaji wa kundi hilo.

Newstimehub

Newstimehub

24 Novemba, 2026

19191018 7dfb 462d a5b3 64c4dd2144f2 1795542200983

Mkuu wa Ujasusi wa wapiganaji wa RSF, Al-Tayeb Jabara, amejiunga na upande wa jeshi la Sudan, vyombo vya habari vimeripoti siku ya Jumanne.

Katika video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na mwanaharkati wa Sudan, Jabara alitangaza uamuzi wake wa kuondoka RSF, akiomba radhi watu wa Sudan kwa kujiunga na kundi hilo la wapiganaji dhidi ya taifa.

“Niko mbele ya watu wa Sudan leo kutangaza kuachana kabisa na vikosi vya wapiganaji,” alisema.

Jabara alisema kuwa awali amewahi kufanya kazi katika ofisi ya kamanda wa RSF Mohamed Hamdan Dagalo, ambaye pia anajulikana kama Hemedti, katika Ikulu mjini Khartoum na baadaye Nyala, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kusini.

Wamepotoshwa kuhusu malengo

Alimshtumu Dagalo na washirika wake kwa kuchangia katika kuiharibu Sudan, akisema kuwa alipotoshwa kuhusu malengo ya kundi hilo.

Aliongeza kuwa agenda halisi ya kundi hilo ilikuwa kumtumikia Dagalo na familia yake huku wakiendeleza maslahi ya mataifa ya kigeni yenye lengo la kugawanya Sudan.

Jabara pia alitangaza utayari wake wa mapambano pamoja na jeshi la Sudan dhidi ya wapiganaji wa RSF.

Alitoa wito kwa wapiganaji wa RSF waliobaki kuachana na Dagalo na kurudi jeshini, akiwataka kuchukua fursa ya msamaha uliotangazwa na mkuu wa Baraza la Mpito la Sudan na mkuu wa majeshi Jenerali Abdel Fattah al-Burhan.