Iran yatoa siku tatu za mapumziko kupisha mazishi ya Ali Khamenei

Ali Khamenei anatarajia kuzikwa Julai 9, katika mji wa Kaskazinimashariki mwa Mashhad, mahali alipozaliwa kiongozi huyo.

Newstimehub

Newstimehub

23 Juni, 2026

1782233854827 hsehw6 356233bb0ac4be55ea95f527c0d9170ffc3c4b72185d6654b611087f4458eb3b

Serikali ya Iran imetangaza siku tatu za mapumziko, kupisha mazishi ya aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa taifa hilo, Ayatollah Ali Khamenei.

“Ibada ya mazishi kwa kiongozi wetu itafanyika Julai 4 na 5, huku mazishi yenyewe yakifanyika Julai 6, na siku hiyo itakuwa ni ya mapumziko katika jiji la Tehran,” alisema Hassan Hassanzadeh, ambaye pia ni kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC), anayehusika na sherehe mbalimbali.

Mapema Jumanne, chombo cha habari cha serikali ya Iran, kilitangaza kuwa Julai 4 na 5 kuwa siku za mapumziko kwa jiji la Tehran, huku nchi nzima ikiingia mapumzikoni Julai 6.

Jiji la Tehran linatarajia kushuhudia watu milioni 20 wakihudhuria mazishi hayo.

Ali Khamenei anatarajia kuzikwa Julai 9, katika mji wa kaskazinimashariki mwa mji wa Mashhad, mahali alipozaliwa kiongozi huyo.

Ibada hiyo ilipangwa kufanyika mwezi Machi, lakini ilisogezwa mbele kufuatia vita katika eneo la Mashariki ya Kati.