Ugonjwa wa Ebola unaendelea kusambaa ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Africa CDC).
Kulingana na taasisi hiyo, ugonjwa wa Ebola ambao uliripotiwa kwa mara ya 17 nchini humo, Mei 15 mwaka huu, umeendelea kusambaa katika majimbo tofauti nchini humo.
Kufikia sasa, majimbo matani nchini humo yameendela kuripoti maambukizi ya ugonjwa wa Ebola.
Majimbo hayo ni pamoja na Ituri, Kivu Kaskazini, Kivu Kusini, Haut -Uele na Tshopo.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), mlipuko huu unaenea kwa kasi zaidi kuliko milipuko yote ya Ebola iliyowahi kutokea, na tayari unachukuliwa kuwa mkubwa zaidi katika historia ya taifa hilo la Afrika ya Kati.
Hadi sasa, vifo zaidi ya 2,128 vimeripotiwa kati ya maambukizi 4,566 zilizothibitishwa, huku mikoa ya Ituri, Kivu Kaskazini, Kivu Kusini, Haut‑Uele na Tshopo ikiwa imeathirika kabla ya Bas‑Uele kuongezwa kwenye orodha.
Maambukizi ya Ebola huenea kupitia kugusa wanyama walio hai au waliokufa walioambukizwa au kwa kugusa ngozi au majimaji ya mwili wa mtu aliyeambukizwa ambaye ana dalili za ugonjwa huo.
Dalili zake ni pamoja na homa, maumivu ya misuli na mwili, maumivu ya kichwa, kikohozi, na koo linalouma, ikifuatiwa na kutapika na kuhara pamoja na kutokwa na damu mdomoni, puani, au viungo vya ndani.















