Simba jike watatu waliokuwa wamehifadhiwa kwenye bustani ya wanyama jijini Tokyo, wanaripotiwa kupoteza maisha kutokana na joto kali lililoikumba nchi hiyo.
Wanyama hao, wenye umri wa kati ya 3 na 15, wanaripotiwa kufa siku ya Jumanne na Jumapili, ndani ya bustani ya wanyama ya Tama, iliyoko jijini Tokyo.
Uchunguzi wa awali, umebainisha kuwa, wanyama hao, walikufa kwa kiu, hali iliyopelekea viungo vyao vya mwili kushindwa kufanya kazi.
Kufikia Julai mwaka huu, bustani hiyo ilikuwa na jumla ya simba 16, wakiwemo madume watano na majike 11.
Julai 23 mwaka huu, bustani hiyo ilisimamisha huduma, baada ya hali za wanyama hao kudhoofika.















