Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja amepatikana na hatia ya kudharau mahakama kutokana na kuweka vizuizi barabarani wakati wa maandmano ya Juni 25, 2026, yale ya Gen Z.
Jaji Patricia Nyaundi siku ya Alhamisi alimpata Kanja kuwajibika kwa vizuizi hivyo katikati mwa jiji la Nairobi licha ya agizo la mahakama kutaka polisi kuwapa wananchi tahadhari kabla ya kuweka vizuizi hivyo.
Jaji aliagiza Kanja afike Mahakama Kuu Septemba 22, 2026, kwa ajili ya kujitetea kabla mahakama kutoa hukumu ya kudharauliwa.
Kesi hiyo ni kutokana na maandamano ya kuadhimisha yaliyotokea wakati wa Juni 2024 kuhusu Mswada wa Fedha, huku walalamikaji wakihoji namna polisi walivyozuia watu kufika katika baadhi ya maeneo ya mji wa Nairobi Juni 25, 2026.
Mahakama ilikuwa imetoa agizo la kutaka polisi iwafahamishe wananchi kabla ya kuweka vizuizi vya kuzuia maandamano hayo.
Hata hivyo, mahakama ilibaini kuwa agizo hizo halikutekelezwa wakati barabara za kuelekea katikati mwa mji zilipowekwa vizuizi Juni 25.















