Air Tanzania yasitisha safari za Moscow kwa sababu za kiusalama

Hatua hiyo inakuja wakati kukiwa na changamoto za kiusalama na usumbufu wa safari za anga katika eneo la Moscow.

Newstimehub

Newstimehub

4 Septemba, 2026

de4b4e42 cd08 483b 95e0 950b4733cbaa 1788507615705

Shirika la Ndege la Air Tanzania limetangaza kusitisha kwa muda safari zake za ndege kwenda na kutoka jijini Moscow, Urusi kuanzia Septemba 4, 2026.

Kwa mujibu wa taarifa ya shirika hilo, uamuzi huo umefikiwa baada ya kufanya tathmini ya mazingira ya uendeshaji wa safari hizo, huku usalama wa abiria, wafanyakazi na ndege ukipewa kipaumbele.

Abiria waliokuwa na tiketi kwenye safari zilizoathiriwa wametakiwa kuwasiliana na Air Tanzania au mawakala wao wa usafiri kwa maelekezo kuhusu kubadilishiwa safari au kurejeshewa fedha, kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa.

Air Tanzania imesema itaendelea kufuatilia hali ya usalama na mazingira ya uendeshaji na kutoa taarifa zaidi kuhusu kurejeshwa kwa safari hizo mara tu itakapoona mazingira yanafaa.

Hatua hiyo inakuja wakati kukiwa na changamoto za kiusalama na usumbufu wa safari za anga katika eneo la Moscow.

Air Tanzania imeomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza kutokana na uamuzi huo na kuwashukuru abiria wake kwa uelewa na ushirikiano.