Polisi nchini Afrika Kusini wameanza msako wa washukiwa watatu baada ya mtangazaji wa zamani wa michezo wa SABC Owen Ndlovu kutekwa nyara na kupatikana ameuawa saa chache baadaye katika mkoa wa Gauteng.
Ndlovu alishambuliwa eneo la Katlehong, East Rand jijini Johannesburg, Jumanne usiku wakati akiwa njia kumchukua mke wake kanisani, msemaji wa polisi Kanali Dimakatso Nevhuhulwi alisema.
Wanaume watatu, mmoja akisemekana kuwa na bastola, waliwakabili wawili hao na kuwashambulia, shirika la habari la taifa la SABC liliripoti.
“Wakati yeye [mke wa Ndlovu] walifika kwenye gari lao, wanaume watatu, mmoja akiwa na silaha, ghafla wakawakabili, na kumsukuma mke wake na kumtaka mume wake aende kwenye kiti cha nyuma cha gari yake. Washukiwa kisha wakaondoka naye kwenye gari,” alisema Nevhuhulwi.
Uchunguzi unaendelea
Polisi wanasema wanaume watatu, mmoja akiwa na silaha, walimkabili.
Mwili wa Ndlovu ulipatikana na wakazi ukiwa umetupwa kando ya barabara katibu na Thokoza Jumatano asubuhi.
“Mwili ulipatikana umetupwa kando ya barabara. Upasuaji utafanyika kubaini chanzo cha kifo,” Nevhuhulwi alisema.
Polisi baadaye walipata gari lake likiwa limeachwa katika eneo la Walkerville, kusini mwa jiji la Johannesburg.
Ndlovu alikuwa maarufu kwa kazi zake za utangazaji wa michezo na kutetea haki za wanamuziki, kuchangia katika maendeleo na kutangaza michezo ya Afrika Kusini na ubunifu.
Polisi walitoa wito kwa yoyote mwenye taarifa ambazo zitaweza kuwatambua au kuwapata waliko kutoa taarifa.















