Waziri Mkuu wa zamani wa China, Zhu Rongji amefariki dunia siku ya Jumatano, akiwa na umri wa miaka 97.
Kulingana na Shirika la Habari la China Xinhua, Rongji amefariki dunia jijini Beijing, akiwa na umri wa miaka 97.
Wakati wa uhai wake, Zhu alikuwa Naibu Waziri Mkuu aliyeshughulikia uchumi wa China, kati ya mwaka 1991 na 1998, kabla ya kuwa waziri mkuu wa tano wa nchi hiyo, kutoka 1998 hadi 2003.
Zhu atakumbukwa kwa msimamo wake mkali dhidi ya ufisadi.















