Iran yakana kuishambulia meli ya Korea Kusini Mlangoni mwa Bahari ya Hormuz

Katika taarifa yake iliyotolewa siku ya Alhamisi, Iran imesema kuwa haihusiki na madai ya jeshi lake kushambulia chombo hicho.

Newstimehub

Newstimehub

7 Mei, 2026

12d69740477ee97fec0a3ab9b5e45c43920463cacb89d11e35ef6af728585f11

Iran, kupitia ubalozi wake ulioko Seoul umekana madai ya kuhusika na kuishambulia na kuiharibu vibaya meli ya Korea Kusini katika Mlango Bahari wa Hormuz.

Katika taarifa yake iliyotolewa siku ya Alhamisi, Iran imesema kuwa haihusiki na madai ya jeshi lake kushambulia chombo hicho.

Badala yake, Iran ilisisitiza kuwa taratibu za uongozaji meli katika eneo hilo, zilikuwa zimeathiriwa na hali ya usalama inayoendelea katika ukanda huo kwa sasa.

Kulingana na Iran, ili upite kwa usalama katika Mlango Bahari huo, ni vyema kanuni na masharti yote kuzingatiwa ipasavyo.

Iran iliahidi kuendelea kusimamia usalama wa vyombo vyote vya majini katika ukanda huo, kulingana na sheria za kimataifa.

Siku ya Jumanne, Shirika la Habari la Korea (Yonhap), liliripoti mlipuko mkubwa kwenye chombo cha HMM Namu katika eneo la Mlango Bahari wa Hormuz.