Ubalozi wa Marekani nchini Kenya watoa tahadhari kuhusu maandamano ya Juni 25

Ubalozi wa Marekani nchini Kenya umetoa tahadhari kwa raia wake kuhusu uwezekano wa kufanyika kwa maandamano katika maeneo mbalimbali Kenya.

Newstimehub

Newstimehub

19 Juni, 2026

d2e14f904334a1c97b050eeccf70475875fd9c212260951c8d6a1c78cd478e71

Ubalozi wa Marekani nchini Kenya umetoa tahadhari kwa raia wake kuhusu uwezekano wa kufanyika kwa maandamano katika maeneo mbalimbali nchini, hasa katika miji mikubwa na katikati mwa jiji la Nairobi, kuelekea kumbukumbu ya tarehe 25 Juni ya maandamano ya kupinga serikali yaliyoshuhudiwa katika miaka miwili iliyopita.

Katika tahadhari hiyo iliyotolewa Alhamisi, ubalozi ulionya kuwa maandamano yanaweza kutokea wakati wowote, ingawa uwezekano wake ni mkubwa zaidi ni itakapokaribia tarehe 25 Juni.

Ubalozi huo ulisema kuwa maandamano hayo yanaweza kusababisha msongamano mkubwa wa magari, kufungwa kwa barabara, na vizuizi vinavyoweza kuwekwa na waandamanaji pamoja na vyombo vya usalama.

“Juni 25 ni kumbukumbu ya maandamano yaliyotokea Kenya katika miaka miwili iliyopita. Maandamano yanaweza kutokea wakati wowote, lakini uwezekano wake ni mkubwa zaidi karibu na Juni 25,” ilisema taarifa hiyo.

Raia wa Marekani wanaoishi au kusafiri Kenya wametakiwa kuwa waangalifu zaidi na kuepuka maeneo ambayo kuna maandamano au mikusanyiko mikubwa ya watu.

Ubalozi huo pia umewashauri kufuatilia vyombo vya habari vya nchini kwa kuhusu hali ya usalama na kuwa waangalifu kuhusu mabadiliko yoyote yanayoweza kuathiri usalama wao na safari zao.

Tahadhari hiyo inakuja wakati kukiwa na matarajio ya maandamano ya kumbukumbu yanayohusishwa na maandamano ya Juni 2024 dhidi ya muswada wa fedha, ambayo yalizua machafuko makubwa na kusababisha maelfu ya Wakenya kuandamana barabarani kupinga mapendekezo ya kodi na masuala ya utawala.