Ajali ya kivuko yaua 95 Zimbabwe

Chombo hicho, ambacho kinatoa huduma za usafiri kati ya mji wa kaskazini wa Kariba na vijiji vya karibu, kilikumbwa na dhoruba kali, kabla ya kupinduka na kuzama ndani ya ziwa hilo.

Newstimehub

Newstimehub

12 Agosti, 2026

6689ae5d 2f70 4711 9169 a254e96dd2d2 1786480014717

Watu 95 wamekufa maji nchini Zimbabwe, baada ya kivuko walichokuwa wakisafiria, kuzama ndani Ziwa Kariba.

Chombo hicho, ambacho kinatoa huduma za usafiri kati ya mji wa kaskazini wa Kariba na vijiji jirani, kilikumbwa na dhoruba kali, kabla ya kupinduka na kuzama ndani ya ziwa hilo.

“Shughuli za uokoaji zinaendelea na tutaendelea kutoa taarifa zaidi kadiri muda unavyokwenda,”ilisema taarifa ya jeshi la polisi la Zimbabwe, siku ya Jumanne.

Kulingana na vyombo vya habari vya nchi hiyo, baadhi ya abiria waliokolewa, japo idadi yao haikuweza kufahamika mara moja.

Ziwa Kariba linapatikana katika mpaka wa Zimbabwe na Zambia, takribani kilomita 300 kutoka mji  mkuu wa Harare.