Trump: Marekani inapigana na Iran kulinda washirika wake Mashariki ya Kati na Magharibi

Trump pia amedai kuwa Iran inaweza kuwa tishio kwa Ulaya na baadhi ya miji ya Marekani katika siku zijazo.

Newstimehub

Newstimehub

3 Septemba, 2026

fbfe30cb ad5f 45da b9eb 90d7fff3c7de 1788420140919

Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema kuwa Marekani inaikabili Iran kwa lengo la kulinda washirika wake wa Mashariki ya Kati pamoja na mataifa ya Magharibi dhidi ya mashambulizi yanayoweza kutokea.

“Tunafanya hivyo kusaidia Mashariki ya Kati. Tunafanya hivyo kusaidia Israel. Na tunafanya hivyo kujilinda wenyewe, kwa sababu baada ya kuiangamiza Israel, jambo ambalo wangelifanya kwa furaha kubwa, na kisha kuishambulia Mashariki ya Kati, wangekuja kuishambulia Ulaya na baadhi ya miji yetu,” alisema Trump Jumatano.

Wakati huo huo, amesema kuwa Marekani “inafanya vizuri sana” katika kukabiliana na Iran. 

Kauli hizo zilitolewa wakati mapigano kati ya Marekani na Iran yalipozuka tena baada ya kipindi cha takribani mwezi mmoja cha utulivu.

Mwishoni mwa wiki, Marekani ilishambulia vitua vya kurusha roketi vilivyokuwa kwenye Kisiwa cha Larak, nchini Iran. Iran ilijibu kwa kurusha makombora kuelekea Jordan na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Siku ya Alhamisi, ving’ora vya tahadhari vilisikika nchini Kuwait, huku mifumo ya ulinzi wa anga ikijaribu kuzuia mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani.

Wizara ya Ulinzi ya Kuwait ilieleza kwenye mtandao wa X kuwa ilikuwa inakabiliana na kile ilichokiita “uchokozi wa wazi wa Iran.”

Mapigano yamezidi kushika kasi tangu jeshi la Marekani liliposhambulia maeneo ya Iran yaliyoko kwenye kisiwa katika Mlango-Bahari wa Hormuz mwishoni mwa wiki. Marekani ilisema ilifanya shambulio hilo kwa sababu Iran ilikuwa inapanga kutumia maeneo hayo kuweka mabomu ya ardhini, baharini.

Iran ilijibu kwa kurusha makombora kuelekea vituo vya kijeshi vya Marekani nchini Jordan, lakini makombora hayo yalinaswa na mifumo ya ulinzi wa anga.