Amesema tuhuma za uongo dhidi ya Uturuki ni jaribio la Israel kuficha “ukatili wake huko Gaza”.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kikao cha Baraza la Mawaziri jijini Ankara siku ya Jumanne, Erdogan alisema: “Hatujali tuhuma za uongo zinazotolewa dhidi ya nchi yetu na mtandao wa wauaji wenye damu ya watu 75,000 wasio na hatia huko Gaza, wengi wao wakiwa watoto na wanawake.”
Rais huyo wa Uturuki alisema tuhuma hizo dhidi yake ni njia ya makusudi ya kugeuza macho ya watu, akisisitiza historia ya Uturuki ya kuwapa hifadhi watu waliokimbia mateso.
“Historia yetu inajumuisha sifa ya kuwapa hifadhi wale waliokimbia mateso ya Wanazi,” alisema Erdogan.
“Wale wanaoisingizia Uturuki ili kuficha ukatili wao huko Gaza wanajua ukweli huo vizuri.”
Rais huyo pia alizungumzia malengo ya Uturuki ya kiteknolojia, akisema kuwa maendeleo ya uwezo wa satelaiti si jambo la hiari tena kwa nchi hiyo.
“Kuhusu Uturuki, kuendeleza uwezo wa satelaiti ni lazima, si hiari,” alisema Erdogan.
Pia alionyesha mshikamano wa Uturuki na Venezuela kufuatia matetemeko mawili makubwa yaliyolikumba taifa hilo, akiahidi msaada kwa watu wa Venezuela “kwa njia zote tunazoweza”.
“Tunatoa msaada wetu kwa watu wa Venezuela, nchi rafiki na ndugu, kwa kila njia zote tunayoweza,” alisema Erdoğan.
Alisema Uturuki ilituma ndege mbili za kijeshi zilizobeba timu za uokoaji pamoja na misaada ya kibinadamu kuelekea maeneo yaliyoathiriwa na tetemeko la ardhi nchini Venezuela, na timu hizo tayari zimeanza kazi kwa kushirikiana na mifumo ya kimataifa ya uokoaji.
“Serikali za mitaa pia zimeanzisha kampeni za misaada kuunga mkono Venezuela,” alisema.















