Polisi nchini Kenya wafunga sehemu ya Nairobi kutokana na mikusanyiko ya kuadhimisha maandamano

Polisi waliweka vizuizi katika barabara kadhaa na kuzuia magari kuingia katika baadhi ya barabara za jiji la Nairobi.

Newstimehub

Newstimehub

25 Juni, 2026

d91adfedb14422d2ec6a2fb370439fc168ae940db94310d7ecccfd86814d5e9e

Polisi nchini Kenya wamefunga sehemu kubwa ya mji mkuu katika kuzuia mikusanyiko ya kuadhimisha miaka miwili ya maandamano ya Gen Z.

Maelfu ya Wakenya waliandamana Juni 2024 dhidi ya hali mbaya ya uchumi na ufisadi, na kufikia kuvamia bunge ili kushinikiza kuondolewa kwa kodi.

Watu wasiopungua 60 waliuawa kulingana na mashirika kadhaa ya haki za binadamu, ikiwemo Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu.

Maafisa wengi wa polisi

Siku ya Alhamisi, polisi Polisi waliweka vizuizi katika barabara kadhaa na kuzuia magari kuingia katika baadhi ya barabara za jiji la Nairobi. Shule na baadhi ya ofisi zimefungwa.

Kuna polisi wengi katikati mwa jiji la Nairobi.

Mapema wiki hii Rais William Ruto alisema kuwa Wakenya wana haki ya kuandamana lakiki akaonya kuhusu yeyote ‘‘anayehamasisha watu kuharibu mali au kusababisha vurugu”.

Naibu wa zamani wa Ruto, Rigathi Gachagua, ambaye sasa ni hasimu wake kisiasa, ameonya vijana wa Kenya kutoandamana Alhamisi kwa kuhofia kuhus hatari kwa maisha yao, akisema: “Nawaomba: kaeni nyumbani.”