Watu wanne wamepatikana na maambukizi ya ugonjwa wa mafua ya ndege nchini Marekani, kulingana na Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) cha nchini humo.
Wagonjwa watatu kati yao, walipatikana katika majimbo ya Washington na Oregon, huku mwingine akipoteza maisha kutokana na ugonjwa huo katika jimbo la Washington.
Mafua ya ndege ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na virusi vya mafua vinavyoathiri ndege zaidi, na mara chache huambukiza wanyama wengine au binadamu.
Maambukizi ya mafua ya ndege huusisha watu wanaofanya kazi moja kwa moja na ndege, ambapo maambukizi yake hupatikana kwa njia ya kuingiliana kwa karibu na ndege wagonjwa, waliokufa, au wanyama walioambukizwa (kama kuku, ndege wa majini, au ng’ombe wa maziwa).















