Serikali ya Kenya imetia saini mkataba wa shilingi bilioni 154.2 (bilionino $1.2) na Kampuni ya China Road and Bridge Corporation wa upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Waziri wa Uchukuzi Davis Chirchir alisema siku ya Jumanne.
Taifa hilo la Afrika Mashariki linalenga kuongeza idadi ya abiria katika uwanja huo wa Nairobi hadi mara tatu kufikisha milioni 22 kutoka milioni 7.5
Mwaka uliopita mradi huo ulisitishwa kutokana na Kenya kufuta makubaliani ya 2024 na kampuni ya India ya Adani Group kufuatia kufunguliwa mashtaka kwa mmiliki wake nchini Marekani.
“Mradi huu unajumuisha ujenzi wa jengo jipya na maeneo mengine, uiimarishaji wa na ukarabati wa miundombinu, matengenezo ya maeneo ya kupaa na kutua ndege,” Chirchir aliandika katika mtandao wa X.
Uwekezaji mkubwa katika sekta ya anga
Kenya inalenga kuendelea na nafasi yake muhimu ya usafiri wa anga katika kanda, huku nchi kama Ethiopia na Rwanda ikiwekeza katika ujenzi wa viwanja vya ndege kwa maandalizi ya kupokea ndege nyingi pamoja na abiria.
Kufikia mwishoni mwa 2025, Uwanja wa Ndege wa JKIA ulihudumia abiria takriban milioni 9, ikiwa ni zaidi ya uwezo wake wa abiria milioni 7.5 kila mwaka, Chirchir alisema.















