Burundi kuajiri walimu wapya 5,000

Mchakato huo wa kuajiri walimu hao wapya, unatarajiwa kuratibiwa na idara za elimu katika wilaya mbalimbali za Burundi.

Newstimehub

Newstimehub

25 Agosti, 2026

cd555e90 bf2c 4f78 b0a5 c2f7ab43352e 1787644929158

Serikali ya Burundi inalenga kuajiri walimu wapya 5,000, ili kuziba pengo na uchache wa walimu katika shule za msingi na sekondari nchini humo.

Uamuzi huo, unafuatia kikao cha baraza la mawaziri la nchi hiyo, kilichoketi hivi karibuni.

Mchakato huo wa kuajiri walimu hapo wapya, unatarajiwa kuratibiwa na idara za elimu katika wilaya mbalimbali za Burundi.

Wizara ya elimu ya nchi hiyo, inatazamia kuajiri walimu 995 wenye shahada ya ngazi D6 ya diploma, 2,538 wenye D7 diploma, 22 wenye A2 diploma, na wengine 1,445 wenye elimu ya vyuo vikuu.

Ili kuhakikisha uwazi katika mchakato huo wa ajira, wizara ya elimu ya Burundi, imesema kuwa itahahakikisha kuwa zoezi hilo linakuwa na ushindani.