Marekani inalaumiwa kwa kusema kimakosa kuwa Ethiopia “ni ya pili kwa uchumi mkubwa barani Afrika” huku akipongeza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili chini ya serikali ya Trump na sera yake ya mambo ya nje ya “Marekani Kwanza”.
Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema katika mtandao wa kijamii Jumatatu, Agosti 24, kuwa ”ushirikiano huu utafanya Marekani iwekeze na kupatikana tija zaidi kwa Wamarekani na Waethiopia kutoka nchi yenye uchumi wa pili kwa ukubwa barani Afrika.”
Watumiaji wa mitandao ya kijamii waliilaumu kwa kusema Ethiopia ni ya pili kwa uchumi mkubwa barani, huku wengine wakisema kuwa taarifa hiyo ni ya kupotosha, na wengine wakisema kuwa maafisa wa Marekani hawana ufahamu wa kutosha kuhusu bara la Afrika.
Ethiopia ni ya tisa kwa uchumi mkubwa barani Afrika, kulingana na takwimu za Shirika la Fedha Duniani (IMF). Mataifa matatu yenye uchumi mkubwa duniani ni Afrika Kusini, Misri na Nigeria.
Makosa haya ya sasa hivi yanakuja wiki kadhaa baada ya Marekani kuchakachua ramani ya Afrika, ikionesha mipaka tofauti ya nchi mbalimbali wakati wa mkutano wa kimataifa nchini Brazil, jambo lilowaghadhabisha wengi.















