Shirika hilo la Fedha limesema siku ya Jumatatu kuwa litatoa Dola milioni 600 kwa Dangote Group ili kusaidia uzalishaji wa mbolea mara tatu nchini Nigeria na kujenga kiwanda kipya nchini Ethiopia.
AFC imesema katika taarifa yake kuwa fedha hizo zitaenda kwa Greenview Fertilizer Corp., kampuni ya Dangote ya mbolea, na kusaidia kuongeza uzalishaji wa mbolea ya urea Nigeria kutoka tani milioni 3 hadi milioni 9 kwa mwaka na kuongeza tani nyengine milioni 3 nchini Ethiopia.
Kampuni ya Dangote Group imesema mradi wa mbolea utagharimu mpaka Dola bilioni 7.
Afrika inaagiza kiwango kikubwa cha mbolea, na kutatiza shughuli za ukulima pindi panapokuwa na migogoro inayotatizo usafirishaji wa mbolea.
Kujenga ‘msingi wa Afrika kujilisha yenyewe’
“Kwa kuunga mkono maendeleo ya kiwanda kikubwa duniani cha mbolea, AFC inasaidia kujenga msingi wa Afrika wa kujilisha yenyewe, kuzalisha ajira na kuimarisha uchumi,” amesema Mkurugenzi Mtendaji wa AFC Samaila Zubairu.
Shirika hilo la fedha ambalo liko jijini Lagos mwanzoni lilisaidia uratibu wa mkopo wa Dola bilioni 3 kwa kiwanda cha Dangote cha kinachosafisha mapipa 650,000 kwa siku, kikubwa Afrika.















