CIA yatilia shaka madai ya Israel ya kushambuliwa kwa Rais Trump

Hapo awali, jarida hilo lilidai kuwa, Rais Trump alihamishwa kwenye ndege nyingine badala ya Air Force One, baada ya kuwepo na hofu ya usalama kwenye ndege mpya ya Boeing 747-8 iliyozawadiwa Marekani na Qatar.

Newstimehub

Newstimehub

13 Agosti, 2026

3da474c6 3bb2 4114 a4f0 a935f13a3c35 1786640084615

Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA)limedai kutilia shaka taarifa za njama za kumuua Rais Donald Trump, kama ilivyotangazwa na Israel.

Likinukuu vyanzo vya kijasusi vya Marekani, jarida la The Washington Post, lilisema kuwa maofisa wa CIA hawakushawishika na taarifa za Israel, kuhusu njama za kutaka kumuua Rais Trump, wakati akitokea kwenye mkutano wa NATO, nchini Uturuki mwezi uliopita.

Hapo awali, jarida hilo lilidai kuwa, Rais Trump alihamishwa kwenye ndege nyingine badala ya Air Force One, baada ya kuwepo na hofu ya usalama kwenye ndege mpya ya Boeing 747-8 iliyozawadiwa Marekani na Qatar.

Inaripotiwa kuwa, Trump alihamishiwa kwenye ndege ya kijeshi aina ya C-32A kwa kutumia gari maalumu la kubebea chakula, kabla ya kupelekwa kwenye kambi ya anga ya Mildenhall.

Licha ya Ikulu ya White House kutokuwa kujibu maswali ya tathmini ya usalama, afisa mmoja wa Marekani alisema kuwa, Rais Trump amekutana na vitisho kadhaa vya usalama wake, ikiwemo la Iran.

“Kama alivyosema mwenyewe, amekumbana na vitisho kadhaa vya kuhatarisha maisha yake na ndio maana hatua zinachukuliwa kumuhakikishia usalama,” alisema afisa huyo.

Hata hivyo, CIA haikuwa tayari kuzungumzia suala hilo, huku Ubalozi wa Israel nchini Marekani, ukishindwa kujibu maswali ya jarida la The Washington Post.

Licha ya maswali kadhaa kuhusu shirika hilo la kijasusi la Marekani limesema kuwa maamuzi magumu yalichukuliwa kama tahadhari.

 “Idara ya Kijasusi imeponea chupuchupu na kiongozi huyu, kwahiyo hatuwezi kubahatisha,” alisema mmoja wa maofisa hao.

Siku ya Jumanne, Trump mwenyewe alisema kuwa ndege nyingine ilitumika kutokana na maamuzi ya Idara ya Kijasusi ya nchi hiyo.

“Ni wajibu wao wanausalama, mimi nafuata kile wanachokielekeza,” alisema Trump.