Zimbabwe: Bunge la Seneti lapitisha muswada wa kumbakisha Mnangagwa madarakani hadi 2030

Jumla ya maseneta 75 walipiga kura ya ndio, kuunga mkono muswada huo ambao utasogeza mbele uchaguzi ujao kutoka mwaka 2028 hadi 2030, na hivyo kumuongezea Mngangagwa miaka miwili zaidi ya kukaa madarakani.

Newstimehub

Newstimehub

25 Juni, 2026

73cb64a2a13a68597e4b69e98e527b1876f51c63fa0d17bb6b3e5e122bee9361

Bunge la Seneti nchini Zimbabwe limepitisha mabadiliko ya katiba ambayo yataondoa uchaguzi wa nafasi ya urais na kuongeza muda wa kukaa madarakani kwa Rais Emmerson Dambudzo Mnangagwa.

Jumla ya maseneta 75 walipiga kura ya ndio, kuunga mkono muswada huo ambao utasogeza mbele uchaguzi ujao kutoka mwaka 2028 hadi 2030, na hivyo kumuongezea Mngangagwa miaka miwili zaidi ya kukaa madarakani.

Ni maseneta wanne pekee, waliopinga muswada huo.

Kati ya mambo mengine, muswada huo unaleta mabadiliko makubwa katika namna ya kuchagua marais, pamoja na kuongeza muda wa madaraka ya marais na wabunge  kutoka miaka mitano hadi saba.

Hata hivyo, wanaharakati wa haki za binadamu nchini humo, wamepinga mfumo huo mpya wakitaka kufanyike kwa kura ya maoni ili muswada huo upite.