Wagonjwa hawajulikani waliko baada ya kituo cha kutibu Ebola kushambuliwa nchini DRC

Ikiwa ni tukio la pili la aina hiyo katika kipindi cha wiki moja, wakazi waliokuwa na hasira walichoma moto kituo cha kutibu Ebola mashariki mwa DRC katika Hospitali ya Rufaa ya Mongwalu.

Newstimehub

Newstimehub

25 Mei, 2026

2a92ad1d9d45a0a32787117e21294c5b60d9354e7aed1ebe2e368bde2787b9a7

Wakazi wa mji wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambao umekumbwa na mlipuko wa Ebola walichoma moto mahema yaliokuwa yanatumika kama vituo vya kutibu watu siku ya Ijumaa, na sasa wagonjwa 13 wa Ebola hawajulikani waliko, kulingana na vyombo vya habari vya eneo hilo.

Ikiwa ni tukio la pili la aina hiyo katika kipindi cha wiki moja, kundi la “vijana waliokuwa na hasira” lilivamia mahema yaliyoekwa na shirika la Madaktari Wasiokuwa na Mipaka (MSF) katika Hospitali ya Rufaa ya Mongwalu, kulingana na ripoti.

Hospitali hiyo ilikuwa na wagonjwa 28 wanaoshukiwa kuwa na maambukizi ya Ebola, na watu wasiopungua 13 walikimbia eneo hilo na hawajulikani waliko, Richard Lokudi, mkurugenzi wa afya wa hospitali ya Mongwalu, ameviambia vyombo vya habari vya eneo hilo.

Aliongeza kuwa polisi walianzisha uchunguzi Jumamosi asubuhi kuwasaka waliohusika na kuwatafuta wagonjwa ambao hawapo, ambao wanaaminika kuwa miongoni mwa watu wa eneo hilo.

Hali imezidi kuwa tete

Shambulio hilo lilikuwa la pili katika kituo cha kutibu Ebola katika kipindi cha wiki moja, kudhihirisha kuongezeka kwa hali kuwa tete kati ya wahudumu wa afya na jamii za maeneo hayo huku kukiwa na mlipuko.

Siku ya Alhamisi, kituo cha kituo cha karibu na mji wa Rwampara kilichomwa moto baada ya jamaa kukatazwa kuchukua mwili wa mtu aliyesemekana kufariki kutokana na Ebola.

Mashirika ya misaada yameonya kuhusu hofu, taarifa za kupotosha ambazo ni kikwazo kwa kukabiliana na ugonjwa huo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo miundombinu dhaifu na ukosefu wa usalama inafanya hali ya mlipuko huo kuwa mbaya zaidi.

Kufikia Jumapili, mamlaka za nchini DRC ziliorodhesha maambukizi 904 huku vifo 119 vikitajwa kusababishwa na ugonjwa huo. Katika nchi jirani ya Uganda, maafisa wamethibitisha maabukizi matano na kifo kimoja.​​​​​​​