Wabunge wa Madagascar wamng’oa spika wao

Zaidi ya theluthi mbili ya wabunge hao, walipiga kura ya kumuondoa Siteny Randrianasoloniaiko kwenye kiti cha uspika.

Newstimehub

Newstimehub

24 Novemba, 2026

15715522 ef4b 4d6b 8794 784879d3e2a8 1795513783602

Wabunge wa Madagascar siku ya Jumanne, walipiga kura ya kumuondoa spika wa Bunge la Taifa la nchi hiyo, kufuatia tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi.

Zaidi ya theluthi mbili ya wabunge hao, walipiga kura ya kumuondoa Siteny Randrianasoloniaiko kwenye kiti cha uspika.

Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 54, anaaminika kuwa na mpango wa kugombea nafasi ya urais kwenye uchaguzi wa mwishoni mwa mwaka 2027, wakati serikali ya mpito ya sasa, itakapokuwa ikimaliza muda wake.

Wabunge hao, wametetea uamuzi wao, wakisema kuwa ulilenga kulinda heshima ya bunge, wakimtuhumu Randrianasoloniaiko kwa kukiuka baadhi ya vifungu vya sheria vinavyoendesha bunge hilo.