Wakati Rais Denis Sassou Nguesso akijiandaa kuunda serikali mpya, mjadala umeibuka kuhusu uongozi wake wa muda mrefu nchini Congo-Brazzaville.
Nguesso ni miongoni mwa viongozi waliokaa madarakani kwa muda mrefu barani Afrika, baada ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2015 kuondoa ukomo wa umri na mihula ya urais, hatua iliyomruhusu kugombea tena.
Ushindi wake mkubwa katika uchaguzi wa hivi karibuni umeibua maswali kutoka kwa baadhi ya wachambuzi kuhusu mustakabali wa demokrasia na ushindani wa kisiasa nchini humo.
Hata hivyo, serikali inaendelea kusisitiza kuwa mabadiliko hayo ni ya kisheria na yanahakikisha uthabiti wa kisiasa na maendeleo ya taifa.
CHANZO: Newstimetr














