Ukraine, Uholanzi zatiliana saini mkataba wa ulinzi wakati wa mkutano wa NATO

Mkataba huo, ulisainiwa kati ya Rais wa Ukraine na Waziri Mkuu wa Uholanzi wakati wa mkutano unaofanyika jijini Ankara

Newstimehub

Newstimehub

7 Julai, 2026

30bb2f9c2d646cfeddc96f0a19e0b8dd4e78775981d1fb44ed136c08c44d5bda

Ukraine na Uholanzi zimetiliana saini mkataba wa kushirikiana kiulinzi.

Mkataba huo ulisainiwa kati ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy na Waziri Mkuu wa Uholanzi Rob Jetten, siku ya Jumanne wakati wa mkutano wa 36 wa NATO, jijini Ankara.

Mbali na mkataba huo, Zelenskyy alikuwa na wasaa wa kukutana na Rais wa Finland Alexander Stubb, Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney, pamoja na Waziri Mkuu wa Estonia Kristen Michal.

Kupitia taarifa yake baada ya kukutana na Zelenskyy, ofisi ya Carney ilisema kuwa, wawili hao walizungumza yanayojiri duniani kwa sasa, ikiwemo na jitihada za kidiplomasia za kumaliza mgogoro kati ya Urusi na Ukraine.