Ripoti mpya yafichua kuwa shirika la ujasusi la SVR limechukua shughuli za ushawishi na propaganda zilizokuwa zinaendeshwa na kundi la Wagner barani Afrika.
Wagner, iliyokuwa ikijulikana kwa mbinu kali na uwepo mkubwa Afrika, ilipeleka wapiganaji katika nchi kama Libya na Mali huku pia ikiendesha kampeni za propaganda na kuvuruga utulivu. Baada ya kifo cha Prigozhin kufuatia jaribio la uasi dhidi ya Moscow, wizara ya ulinzi ya Urusi ilianzisha muundo mpya unaoitwa “Africa Corps” kuratibu operesheni za usalama.
Hata hivyo, uchunguzi wa vyombo vya habari vya kimataifa umebaini kuwa SVR sasa inaongoza shughuli za ushawishi, zikiwemo propaganda, kulinda maslahi ya kisiasa na kiuchumi ya Moscow na kuondoa ushindani barani Afrika na kwingineko.
Chanzo: Africanews














