Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) cha nchini Tanzania, Tundu Lissu, amefikishwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam , kwa ajili ya kusikiliza hukumu ya kesi ya uhaini inayomkabili.
Hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa na jopo la majaji watatu wanaosikiliza kesi hiyo, likiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, akisaidiwa na James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde.
Lissu anakabiliwa na kesi ya uhaini kufuatia tukio la kukamatwa kwake Aprili 9, 2025 mkoani Mbinga na kufunguliwa mashtaka rasmi.
Kesi hiyo inahusiana na hotuba aliyoitoa mnamo Aprili 3, 2025, wakati chama cha CHADEMA kikiwa kwenye kampeni yake ya “No Reforms, No Election”.
Wakati huo huo, hali ya ulinzi imeimarishwa katika eneo hilo wakati wananchi na watu wengine wanaofuatilia mwenendo wa kesi hiyo wakisubiri hatua inayofuata ya mchakato wa kimahakama.















