Tanzania: Young Africans yaitolea macho mechi dhidi ya Azam FC

Young Africans itamenyana na Azam FC, Juni 24, 2026 katika uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Newstimehub

Newstimehub

23 Juni, 2026

bcb1fa679fb02554f2e49a1a6e037fc569a9b338fc01cc0ad07f583609663f19

Msemaji wa klabu ya Young Africans ya nchini Tanzania, Ali Kamwe, amesisitiza umoja ndani ya klabu hiyo, inapojiandaa na mchezo wa wake dhidi ya Azam FC katika Ligi Kuu ya NBC.

Kulingana na Kamwe, lengo kubwa ni  kuhakikisha timu hiyo inamaliza msimu kwa mafanikio na kutetea ubingwa wake.

Aliongeza kuwa, kila mchezo uliobaki una umuhimu mkubwa kwa Yanga na hakuna nafasi ya kufanya makosa, kwani kupoteza pointi katika hatua hii ya mwisho kunaweza kuathiri malengo yao ya kutwaa taji la ligi.

“Tunatakiwa kushikamana kuhakikisha tunafanya vizuri katika michezo hii iliyosalia. Tutaumia sana tukiangusha pointi na kupoteza ubingwa,” amesema Kamwe.

Young Africans itamenyana na Azam FC, Juni 24, 2026 katika uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.