Ulimwengu

b0debe2c ecf3 4ab4 af35 395995a730c1 1787306037390

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan arudishwa jela baada ya kutoka hospitali

Siku ya Jumanne, Mahakama Kuu ya nchi hiyo, iliamuru Khan, mwenye umri wa miaka 73, apelekwe katika hospitali binafsi ya Shifa iliyoko jijini Islamabadm kwa ajili ya kuchukuliwa vipimo vya afya.

Uko pamoja nasi au dhidi yetu: Marekani yataka ushirikiano wa China dhidi ya Iran

Waziri wa Hazina wa Marekani, Scott Bessent, amesema nchi nyingine zinapaswa kuunga mkono hatua zinazochukuliwa na Marekani au zikabiliwe na matokeo.

Upinzani Kenya wataka ICC ichunguze ghasia za kisiasa na uhalifu wa magenge

Martha Karua amesema ICC inapaswa kuangalia upya mashtaka yaliyowahi kuwasilishwa dhidi ya Rais Ruto na kutathmini iwapo kesi hiyo inapaswa kufunguliwa tena.

Ufaransa yapitisha sheria ya ‘kusaidia watu kufa’

Chini ya sheria hiyo, wagonjwa watakuwa na haki ya kupewa dawa maalumu ambayo itaongeza kasi ya kifo kwa mgonjwa husika, ili kumuondolea mateso.

Afrika

88bab9a5 4c20 4bde 954c d4279616ad08 1787304760435

Mashambulizi ya RSF yaua watu 6, zaidi ya 1,000 wafurushwa Sudan: Ripoti

Mashambulizi katika vijiji 2 kusini-magharibi mwa mji mkuu wa Kordofan Kaskazini yasababisha makumi ya watu kuhama makazi yao.

Tanzania: Tundu Lissu ana kesi ya kujibu

Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu amekutwa na kesi ya kujibu katika kesi ya uhaini inayomkabili inayoendelea katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ya Dar es Salaam.

Watu wasiopungua 40 wafariki katika ajali ya boti jimbo la Sokoto nchini Nigeria

Boti lilizama katika jimbo la kaskazini magharibi la Sokoto nchini Nigeria, miili 40 ya watoto imepatikana kufikia sasa, afisa mmoja wa eneo hilo alisema siku ya Alhamisi.

Wachimba migodi Ghana wataka fedha zao $34.5 milioni zilokwama kutolewa

Chama cha Wafanyakazi wa Migodi nchini Ghana kinasema fedha zilizoko kwenye mfuko wa akiba na za kiinua mgongo ni za wafanyakazi zaidi ya 19,000.