Spika wa Bunge la Senegal amesema mwishoni mwa juma kuwa anajiuzulu, siku mbili baada ya mshirika wake mkubwa kufutwa kazi kama waziri mkuu, hatua inayoongeza mgogoro wa kisiasa katika taifa hilo la Afrika Magharibi.
Hatua ya spika El Malick Ndiaye inafungua njia kwa waziri mkuu aliyefutwa kazi Ousmane Sonko kugombea nafasi hiyo ya spika wa bunge, ambapo chama chake kina idadi kubwa ya viti, hatua ambayo itampa changamoto Rais Bassirou Diomaye Faye.
Manaibu wameitwa kwenye kikao cha bunge kitakachofanyika Jumanne ili kumrudisha Sonko kama mbunge na kumchagua kuwa spika, imesema taarifa rasmi iliyochapishwa Jumapili.
Hii itafanya jitihada za Rais Faye za kuleta mabadiliko kuzidi kuwa ngumu, baada ya kumfuta kazi aliyekuwa mshirika wake Sonko baada ya miezi kadhaa ya hali ya wasiwasi.
Faye ushindi wake mkubwa wa urais ni kupitia Sonko, ambae angeweza kuchukua nafasi ya kuongoza nchi hiyo kama asingezuia kugombea kutokana na kesi ya kashfa.
‘Uongozi uliofeli’
Chama chao cha Pastef kilishinda uchaguzi wa 2024 kufuatia ahadi ya mabadiliko ya kisiasa, baada ya kuahidi kupambana na rushwa katika uchumi ambao ulikuwa na madeni.
Sonko alikuwa na ushawishi mkubwa hasa kutoka kwa vijana kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2024.
Licha ya ushawishi wa Sonko, Faye alishinda kama Rais.
Lakini katika miezi ya hivi karibuni, uhusiano kati ya Faye na mkufunzi wake ulidorora.
Na kadri uhusiano wao ulivyozorota, ndivyo umoja wao wa serikali ulivyovurugika.
Sonko amekuwa akimlaumu Faye kwa “uongozi uliofeli.”
Mara kadhaa pia amekuwa akilalamikia kile alichokiita kasi ndogo ya kupambana na maafisa mafisadi waandamizi waliokuwa katika serikali iliyopita.
Wawili hao pia wametofautiana kuhusu jinsi ya kutatua tatizo la deni kubwa la nchi.
















