Afrika kuwa na mabilionea 10 tu zaidi katika kipindi cha miaka mitano ijayo

Afrika itakuwa na mabilionea 10 zaidi wa thamani ya dola ya Marekani kufikia 2031, Ripoti ya kukadiria Utajiri ya Shirika la Knight Frank ya 2026 imeonesha.

Newstimehub

Newstimehub

4 Juni, 2026

de7b0681755431a36f614d1b511458e3b19eb4a6b0fa475ab5bbd7ddc9a4de5f

Afrika itakuwa na mabilionea 10 pekee zaidi wa thamani ya dola ya Marekani kufikia 2031, Ripoti ya kukadiria Utajiri ya Shirika la Knight Frank ya 2026 imeonesha.

Kwa sasa, bara hilo lina watu 27 wenye utajiri wa zaidi ya dola bilioni 1, wakiongozwa na mfanyabiashara tajiri wa saruji,sukari na mafuta raia wa Nigeria, Aliko Dangote, ambaye kufikia Juni 4, 2026, alikuwa na utajiri wa dola bilioni 36.8 billion, kulingana na ripoti ya Mabilionea ya Bloomberg.

Kukuwa huku kwa mabilionea 10 katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2026-2031), inaonesha sawa na ilivyokuwa kwa Afrika kati ya 2021 na 2026, ambapo ni mabilionea 9 tu waliongezeka, na idadi hiyo kupanda kutoka 18 hadi 27.

Kwa sasa (2026), eneo la Asia ya Pasifiki ndiyo lenye idadi kubwa ya mabilionea duniani — 1,116 kati ya 3,110, kote duniani karibu asilimia 36% ya matajiri ulimwenguni.

Afrika Kusini ina matajiri wengi Afrika

Ripoti ya Knight Frank pia imeonesha kuwa Afrika Kusini, Misri, na Morocco ina idadi kubwa ya matajiri barani Afrika wakiwa na utajiri wa wastani wa mtu mmoja usiopungua dola milioni 30.

Kulingana na ripoti ya Knight Frank, kwa sasa Afrika Kusini ina matajiri wa kiwango hicho 1,347, na wanatarajiwa kuongezeka hadi 1,564 kufikia 2031.

Kwa upande mwingine, Misri, ina watu 822 wa kiwango hicho cha utajiri, na kutarajiwa kuongezeka hadi 977 kufikia 2031.

Kulingana na Knight Frank, teknolojia, kilimo, madini, burudani, michezo, na fedha ndiyo vyanzo vikuu vya kupata utajiri duniani.