Rais wa Liberia Joseph Boakai amewafuta kazi maafisa kadhaa wa serikali na kuagiza kufanyike uchunguzi kufuatia kupatikana kwa kiwango kikubwa cha dawa za kulevya katika miezi ya hivi karibuni jambo lililosababisha wananchi kutaka hatua kali zaidi kuchukuliwa.
Boakai aliwafuta kazi maafisa 12, kutoka kwa msimamizi wa uwanja wa ndege hadi kwa maafisa waandamizi wa usalama, kulingana na taarifa iliyotolewa Alhamisi usiku.
Mapema mwezi huu, mamlaka zilipata tani karibu nne za dawa za kokeni zenye thamani ya dola milioni 317 katika operesheni kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Roberts, karibu kilomita 30 kutoka mji mkuu Monrovia.
Hii ni baada ya operesheni nyingine iliyosababisha kupatikana kwa kilo 238 za kokeni zenye thamani ya dola milioni 19 ambazo zilikuwa zinapitishwa kama mzigo wa biashara, ikiwemo viungo, katika uwanja wa ndege mwezi Juni.
Kufutwa kazi mara moja
Afrika Magharibi ni njia inayotumika kwa kokeni inayotoka Marekani ya Kusini na kupelekwa barani Ulaya, kulingana na wanaofuatilia.
Miongoni mwa naibu mkurugenzi wa shughuli za uwanja wa ndege; kamishna wa polisi wa anayesimamia uchunguzi wa makosa ya jinai, maafisa wa ujasusi na Interpol; na naibu mkurugenzi wa usimamizi wa Shirika la Ujasusi nchini humo (NSA).
Boakai pia aliwafuta kazi “maafisa wote wa serikali na wa usalama wanaotuhumiwa” katika upatikanaji wa dawa hizo za kulevya, taarifa ilisema.















