Rais wa Kenya William Ruto aanza ziara rasmi Tanzania

Rais wa Kenya William Ruto amewasili nchini Tanzania ambapo atafanya ziara rasmi ya siku mbili.  Rais Ruto, amepokelewa na mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan katika ikulu ya jijini Dar es Salaam.

Newstimehub

Newstimehub

4 Mei, 2026

74328a5cdf7109fa7e8985208c38a568895383e7a5866e608659da7155e22daf

Rais wa Kenya William Ruto amewasili nchini Tanzania ambapo atafanya ziara rasmi ya siku mbili.  Rais Ruto, amepokelewa na mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan katika ikulu ya Dar es Salaam.

Viongozi hao wawili wanatarajiwa kufanya mazungumzo ya ana kwa ana, ambapo mambo kadhaa yatajadiliwa. Miongoni mwao, ni pamoja na ushirikiano wa kidiplomasia na uchumi.

Katika ziara hiyo, Rais Ruto pia anatarajiwa kuhudhuria Jukwaa la Wafanyabiashara, na hatimae kulihutubia Bunge la nchi hiyo huko jijini Dodoma, katikati mwa Tanzania.