Mvua kubwa kunyesha katika mikoa 20 nchini Tanzania

Mamlaka ya Hali ya Hewa ya Tanzania (TMA) imeonya kuwa mvua kubwa zitanyesha katika mikoa ya 20 ya nchini humo.

Newstimehub

Newstimehub

29 Desemba, 2025

8aa6e973321fcd479209ed234693fb0fb9ae5d71e46332cc93d1d08cfae4de5f

Katika taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo, TMA iliorodhesha mikoa hiyo ambayo itaathirika na mvua kubwa kuwa Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Kigoma, Katavi, Singida, Dodoma, Rukwa, Songwe na Morogoro.

Mikoa mingine ambayo pia yamewekwa kwenye tahadhari ni Ruvuma, Tanga, Dar es Salaam, Pwani ikiwemo Kisiwa cha Mafia, Lindi, Mtwara, pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba. Mamlaka ya Hali ya Hewa inasema mvua kubwa inaweza kuleta athari mbalimbali.

Miongoni mwa athari zinazotabiriwa ni mafuriko, maporomoko na kutatiza shughuli za uchumi na za kijamii za watu.

Wito umetolewa kwa wakazi katika maeneo yatakayoathirika, hasa wale wanaoishi katika maeneo yenye hatari zaidi, kuchukuwa hatua za kujikinga ili kupunguza athari itakayosababishwa na mvua hizo.

Mamlaka ya Hali ya Hewa pia ilitoa wito kwa umma kufuatilia taarifa watakazokuwa wakitoa mara kwa mara ili waweze kuchukuwa hatua zinazostahiki kuepuka maafa. TMA pia imeonya kuhusu maeneo mengine kuendelea kupata mvua.