Mke wa Besigye awataka viongozi wa Afrika wazungumzie masuala ya haki za binadamu

Katika ujumbe kupitia mtandao wa X, Byanyima alisema aliibua suala la kuendelea kuzuiliwa kwa Dk. Besigye nchini Uganda.

Newstimehub

Newstimehub

24 Septemba, 2026

6cf81dc8 0fa6 434c 8a95 6b5e85e91416 1790244083681

Mke wa mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye na Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS, Winnie Byanyima, amesema alikutana na Rais wa Kenya, William Ruto, pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UNGA), ambapo walijadili masuala ya uzalishaji wa dawa na teknolojia za afya barani Afrika.

Katika ujumbe kupitia mtandao wa X, Byanyima alisema aliibua suala la kuendelea kuzuiliwa kwa Dk. Besigye nchini Uganda.

Kwa mujibu wa Byanyima, Besigye alitekwa jijini Nairobi mwezi Novemba 2024, akapelekwa nchini Uganda ambapo anaendelea kuzuiliwa tangu wakati huo.

Byanyima pia alimtaja Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, akisema anapaswa kuwajibika kisiasa kuhusu tukio hilo, hasa kutokana na Besigye kufikishwa mbele ya mahakama ya kijeshi nchini Uganda na kuendelea kuwekwa kizuizini.

Aidha, Byanyima aliwataka viongozi wa Afrika kuzungumzia hadharani masuala ya utekaji, mateso ya kisiasa, haki za binadamu na kuheshimu utawala wa sheria.