Mashabiki wa soka pamoja na wadau mbalimbali duniani wameendelea kutuma salamu za pole na kumtakia nafuu ya haraka Alex Ferguson baada ya kulazwa hospitalini kwa uchunguzi wa tahadhari.
Mitandao ya kijamii imejaa ujumbe wa kumuombea afya njema kocha huyo wa kihistoria wa Manchester United, huku wengi wakikumbusha mchango wake mkubwa katika soka la dunia.
Ferguson anachukuliwa kuwa mmoja wa makocha bora zaidi katika historia ya mchezo huo baada ya kutwaa mataji 38 akiwa Manchester United.
CHANZO: Newstimetr














