Kuongezwa kwa uzalishaji wa mafuta na kujiondoa kwa UAE kunaweza kuathiri soko la dunia
Sekta ya mafuta duniani imekumbwa na mabadiliko makubwa baada ya OPEC+ kuongeza uzalishaji wake huku Umoja wa falme za kiarabu ikitangaza kujiondoa katika muungano huo.
Hatua ya kuongeza uzalishaji inalenga kuhakikisha upatikanaji wa mafuta unakidhi mahitaji ya soko, hasa katika kipindi ambacho dunia inakabiliwa na mabadiliko ya kiuchumi.
Kwa upande mwingine, kujiondoa kwa UAE kunaweza kudhoofisha mshikamano wa muungano huo na kuleta mabadiliko katika mikakati ya uzalishaji wa mafuta.
Wachambuzi wanasema kuwa hali hiyo inaweza kusababisha mabadiliko ya bei ya mafuta na kuongeza ushindani kati ya wazalishaji wakubwa duniani.
Mwelekeo wa soko la mafuta katika miezi ijayo utategemea jinsi nchi mbalimbali zitakavyokabiliana na mabadiliko haya.
Chanzo.Newstimetr














