China imewaambia raia wake kuondoka Eswatini mara moja, ikitaja ukosefu wa usalama kutoka taifa hilo la Afrika.
Eswatini, zamani ikijulikana kama Swaziland, ni miongoni mwa nchi 12 washirika wa Taiwan ambayo inadai kuwa taifa huru. China inadai kuwa Taiwan ni sehemu yake na kupinga majaribio ya kisiwa hicho kuwa na uhusiano wa kimataifa na mataifa mengine.
Rais wa Taiwan Lai Ching-te alisafiri kwenda Eswatini mwezi Mei, huku Taiwan ikiishtumu China kwa kujaribu kutatiza safari hiyo kwa kushinikiza mataifa ya karibu kuondoa vibali vya ndege kutumia anga zao.
‘Hatari ya usalama’
Wizara hiyo ilitaja “utapeli wa mitandaoni na uhalifu wa kamari” kuwa miongoni mwa matatizo yaliyoko kuhusu usalama.
Haikufahamika haraka raia wangapi wa China wanafanya kazi au kuishi Eswatini.
“Wale wanaosisitiza kusafiri au kuendelea kuishi katika maeneo hayo watakabiliwa na hatari ya usalama, na huenda wakachelewa kupata msaada kutoka kwa ubalozi,’’ wizara hiyo ilisema katika taarifa iliowekwa kwenye mtandao wa kijamii wa WeChat.
Mei 1, China iliendeleza sera yake ya kutotoza ushuru kwa mataifa yote ya Afrika isipokuwa Eswatini.















