Umoja wa Afrika umeonya kuwa kutengwa kwa Afrika Kusini katika majukwaa ya G20 kunadhoofisha sauti ya bara la Afrika katika maamuzi ya kimataifa kuhusu uchumi, maendeleo na mabadiliko ya tabianchi.
Maafisa wa AU wanasema Afrika Kusini imekuwa sauti kuu ya bara hilo ndani ya G20, hasa katika ajenda za maendeleo endelevu, fedha za hali ya hewa na mageuzi ya mfumo wa kifedha wa dunia.
Wachambuzi wanaonya kuwa mgogoro huo unaweza kuathiri nafasi ya Afrika katika majadiliano ya kimataifa ikiwa hautapatiwa suluhisho la kidiplomasia mapema.
CHANZO: Newstimetr














